• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2022

  MAN UNITED YAIPIGA OMONIA NICOSIA 1-0 OLD TRAFFORD


  BAO la mtokea benchi, Scott McTominay dakika ya 90 na ushei limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Omonia Nicosia ya Cyprus katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Kwa matokeo hayo, Man United inafikisha pointi tisa, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na Real Sociedad, wakati Omonia Nicosia inaendelea kushika mkia ikiwa haina pointi nyuma ya Sheriff yenye pointi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAIPIGA OMONIA NICOSIA 1-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top