• HABARI MPYA

  Saturday, October 22, 2022

  GEITA GOLD YAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 NYANKUMBU


  TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Said Ntibanzokiza kwa penalti dakika ya 18 na Offen Chikola dakika ya 53, wakati la Namungo FC limefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 12.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 10 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tisa,  wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 11 za mechi saba nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top