• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2022

  SERENGETI GIRLS YAWACHAPA UFARANSA 2-1 KOMBE LA DUNIA


  TANZANIA imeonyesha uimara katika michuano ya Kombe la Dunia Wasichana U17 baada ya kuwachapa Ufaransa mabao 2-1 leo katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Jawaharlal Nehru, Margao, Goa nchini India.
  Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana Mnally dakika ya 16 na Christer Bahera dakika ya 56 kwa penalti, wakati la Ufaransa limefungwa na Lucie Calba dakika ya 75 na sasa watateremka tena dimbani Jumanne kukamilisha mechi zao za Kundi D kwa kumenyana na Canada.
  Ikumbukwe Serengeti Girls ilianza vibaya michuano hiyo kwa kuchapwa 4-0 na Mabingwa watetezi, Japan. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YAWACHAPA UFARANSA 2-1 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top