• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2022

  KMC YAIBAMIZA MTIBWA SUGAR 2-1 UHURU


  WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC yamefungwa na Ibrahim Ame dakika ya 39 na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 58, baada ya Charles Ilfamya kuanza kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya 12.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake tisa nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAIBAMIZA MTIBWA SUGAR 2-1 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top