• HABARI MPYA

  Saturday, October 08, 2022

  HAALAND AENDELEZA MOTO WA MABAO MAN CITY YASHINDA 4-0


  WENYEJI, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Southampton mabao 4-0 leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na João Cancelo dakika ya 20, Phil Foden dakika ya 32, Riyad Mahrez dakika ya 49 na Erling Haaland dakika ya 65 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 20, sasa wakizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi nane.
  Southampton wao kwa upande wao baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao saba za mechi nane pia nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND AENDELEZA MOTO WA MABAO MAN CITY YASHINDA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top