• HABARI MPYA

  Saturday, October 22, 2022

  TANZANIA YATOA SARE YA 1-1 NA NIGERIA DAR KUFUZU AFCON U23


  TANZANIA imelazimishwa sare ya 1-1 na Nigeria jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya kwanza Raundi ya Pili ya mchujo wa kuwania tiketi ya AFCON U23 mwakani.
  Wageni walitangulia kwa bao la penalti la nyota wa CD Diocesano ya Hispania, Success Makanjuola dakika ya 28, kabla ya mshambuliaji wa Moroka Swallows ya Afrika Kusini, Ally Msengi kuisawazishia Manyara Stars dakika ya 76 kwa penalti pia.
  Timu hizo zitarudina Oktoba 27 nchini Nigeria na mshindi wa jumla atamenyana na Uganda katika mechi ya mwisho y mchujo ya kuwania tiketi ya AFCON U23 mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATOA SARE YA 1-1 NA NIGERIA DAR KUFUZU AFCON U23 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top