• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2022

  MBEYA CITY YATOKA NYUMA NA KUICHAPA POLISI 3-1


  WENYEJI, Mbeya City wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hassan Nassor dakika ya 50, Sixtus Sabilo dakika ya 64 na Tariq Seif dakika ya 73 baada ya Vitalis Mayanga kuanza kuifungia Polisi dakika ya 16.
  Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya sita, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake zake mbili ikiendelea kushika mkia baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YATOKA NYUMA NA KUICHAPA POLISI 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top