• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2022

  AUBAMEYANG AFUNGA CHELSEA YASHINDA 2-0 UGENINI


  TIMU ya Chelsea imepata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Chelsea AC Milan katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, Italia.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na  Jorginho kwa penalti dakika ya 21 na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 34, huku Milan wakimaliza pungufu kufuatia Fikayo Tomori kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 18 kwa kumchezea rafu Mason Mount akiwa kwenye nafasi ya kufunga.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi saba na kupanda juu kwenye msimamo ikiizidi pointi moja Salzburg, wakati Milan inayobaki na pointi nne sawa na washika mkia, Dinamo Zagreb inashukia nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG AFUNGA CHELSEA YASHINDA 2-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top