• HABARI MPYA

  Tuesday, October 11, 2022

  MBEYA CITY YAINGIA ANGA ZA KIMATAIFA


  MARA baada ya pazia la Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2022-23 (TPL) pamoja na Ligi kuu ya Uingereza (EPL) kufunguliwa siku za hivi karibuni, Klabu ya Mbeya City, Chelsea, Aston Villa, Newcastle United pamoja na Leicester City zaingia kwenye udhamini mpya na wa kipekee na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Parimatch inayoendesha shughuli zake nchini.

  Hayo yamebainishwa na Afisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed na kusema  kwamba wamejipanga vilivyo katika kukuza na kuleta changamoto mpya kwenye soka la Tanzania kwa kuangalia katika kushirikisha vilabu vya ndani na nje ya nchi.

   

  “Tunafuraha kubwa kutangaza kuwa washirika na Newcastle United, Leicester City, Aston Villa pamoja na Chelsea, uhusiano huu utakuwa muhimu kwa pande zote kwa namna moja ama nyingine. Hii imekuwa desturi yetu Parimatch kushirikiana na vilabu vikubwa vya soka duniani kama mtakumbuka vizuri huu ni muendelezo tu kwani tulishawahi kufanya kazi na vilabu hivi katika msimu uliopita, lakini pia tumekuwa wa kwanza kuweka historia kwa Tanzania kufanya hivyo”, amesema Ismael.

   

  Mbali na hayo, ni dhahiri tunaenda kuiona Mbeya City katika ‘level’ zingine ndani ya msimu huu licha ya kwamba, imepoteza mchezo wake mmoja muhimu ambao amecheza akiwa katika dimba la nyumbani la Sokoine dhidi ya ‘Waoka mikate wa Vingunguti’ Azam FC.

   

  Kila kitu ni muda kama na tunategemea mchezo unaofuata wa Oktoba 14 dhidi ya Polisi Tanzania  utakaochezwa katika dimba lao la nyumbani Sokoine ataondoka na alama 3 kibindoni na kuanza kasi ya kutafuta ubingwa wa msimu huu, hakuna kinachoshindikana katika soka kila kitu ni jitihada na mbinu kali za kupambana na mpinzani.

  Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni kwenye kasino na michezo ya virtual, Parimatch ipo zaidi ya nchi 15 duniani kote ikiwa na mamilioni ya wateja. Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye michezo, Kasino na Michezo ya virtual. 

  Mbali na soka, kampuni pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAINGIA ANGA ZA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top