• HABARI MPYA

  Thursday, October 27, 2022

  AZAM FC YAIPIGA SIMBA 1-0 BAO PEKEE LA PRINCE DUBE


  BAO la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 36 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nana na kusogea nafasi ya nne,  ikizidiwa wastani wa mabao tu na Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Mabingwa watetezi, Yanga wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 17 za mechi saba, wakifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 za mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA SIMBA 1-0 BAO PEKEE LA PRINCE DUBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top