• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2022

  KILA LA HERI SIMBA, YANGA NA AZAM KESHO


  BODI ya Ligi imezitakia kila heri timu za Azam FC, Simba na Yanga katika mechi zao za marudiano michuano ya Afrika kesho.
  Ni Simba pekee yenye matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Primiero de Agosto nchini Angola katika mchezo wa kwanza Hatua ya makundi ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa.
  Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 na Al  Hila nyumbani katika mchezo wa kwanza 32 Bora Ligi ya Mabingwa na Azam FC ilifungwa 3-0 nchini Libya na Al Akhdar katika 32 Bora ya Kombe la Shirikisho.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA LA HERI SIMBA, YANGA NA AZAM KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top