• HABARI MPYA

  Saturday, October 08, 2022

  MBEYA CITY YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA IHEFU SC SOKOINE


  WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mbeya City walitangulia na bao la Sixtus Sabilo dakika ya nne tu, kabla ya Jaffary Kibaya kuisawazishia Ihefu SC dakika ya 12.
  Kwa matokeo hayo, Mbeya City wanafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 11, wakati Ihefu SC sasa ina pointi mbili, ingawa inaendelea kushika mkia baada ya timu zote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA IHEFU SC SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top