• HABARI MPYA

  Sunday, October 30, 2022

  SIMBA SC YAIFUMUA MTIBWA SUGAR PUNGUFU 5-0 DAR


  WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mzawa Muzamil Yassin dakika ya 38, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 48 na 90 na ushei na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri mawili pia, dakika ya 63 na 73.
  Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi nane, wakati Mtibwa Sugar inayobaki na pointi zake 15 za mechi 10 wanashukia nafasi ya nne.
  Dalili mbaya kwa Mtibwa Sugar zilianza mapema tu dakika ya 37 baada ya kipa wake wa kwanza, Farouk Shikaro kuumia na kushindwa na kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Hamadi Kadedi.
  Hali ikawa mbaya zaidi baada ya walinzi wake wawili wa kati kutolewa kwa kadi nyekundu wote mmoja kila kipindi, Mkongo Paschal Kitenge dakika ya 41 na Cassin Ponera dakika ya 67.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUMUA MTIBWA SUGAR PUNGUFU 5-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top