• HABARI MPYA

  Friday, October 21, 2022

  SINGIDA BIG STARS YAIPIGA KAGERA SUGAR 2-1 PALE PALE KAITABA


  TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Bruno Gomez yote dakika ya 51 na 88, wakati la Kagera Sugar limefungwa na mshambuliaji wake Mganda, Hamisi Kiiza dakika ya 15.
  Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 11 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya saba, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake nane za mechi nane nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAIPIGA KAGERA SUGAR 2-1 PALE PALE KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top