• HABARI MPYA

  Thursday, October 06, 2022

  HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YAUA 5-0


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya FC Copenhagen katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Erling Haaland mawili dakika ya saba na 32 akifikisha jumla ya mabao 19, mengine Davit Khocholava alijifunga dakika ya 39, Riyad Mahrez dakika ya 55 kwa penalti na Julian Alvarez dakika ya 76.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Borussia Dortmund baada ya wote kucheza mechi tatu sawa na Sevilla na FC Copenhagen zenye pointi moja kila moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YAUA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top