• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2022

  KAGERA SUGAR YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 KIRUMBA

   


  WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Hamisi Kiiza dakika ya tisa na Anuary Jabir dakika ya 69, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Rashid Juma dakika ya 27.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi nane katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya 12, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 10 za mechi nane nafasi ya sita.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top