• HABARI MPYA

  Friday, October 21, 2022

  AZAM FC YACHAPWA 2-1 NA KMC UWANJA WA UHURU


  WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC yamefungwa na Nzigamasabo Steve dakika ya 15 na George Makang’a dakika ya 57, wakati la Azam FC limefungwa na Idris Mbombo dakika ya 18.
  Kwa ushindi huo, KMC wanafikisha pointi 13 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tatu, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 11 za mechi saba nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 2-1 NA KMC UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top