• HABARI MPYA

  Monday, October 24, 2022

  SINGIDA STARS YAIZIMA IHEFU 1-0 LITI


  BAO pekee la Shafiq Batambuze dakika ya 17 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Kwa ushindi huo, Big Stars inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Simba na Yanga, ambazo hata hivyo zimecheza mechi sita kila timu.
  Kwa upande wao, Ihefu SC wanabaki na pointi zao tano za mechi nane pia katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA STARS YAIZIMA IHEFU 1-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top