• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2022

  ARSENAL YAPUNGUZWA KASI ENGLAND, SARE 1-1 NA SOUTHAMPTON


  WENYEJI, Southampton wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa St Mary’s, Southampton, Hampshire.
  Wageni walitangulia kwa bao la Granit Xhaka dakika ya 11, kabla ya Stuart Armstrong kuisawazishia Southampton dakika ya 65.
  Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 28 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 11.
  Kwa upande wao, Southampton inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 12 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPUNGUZWA KASI ENGLAND, SARE 1-1 NA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top