• HABARI MPYA

  Monday, October 17, 2022

  SALAH AIINUA LIVERPOOL, YAIPIGA MAN CITY 1-0


  BAO pekee la Mohamed Salah dakika ya 76 jana lilitosha kuipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 13 katika mchezo wa tisa na kujivuta nafasi ya nane, wakati Man City inabaki na pointi zake 23 nafasi ya pili, ikizidiwa pointi nne na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 10.
  Kocha wa Wekundu hao Anfield, Mjerumani Jurgen Klopp alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu kwa kumtolea maneno yasiyofaa refa wa akiba kufuatia Salah kuchezewa rafu mwishoni mwa mchezo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AIINUA LIVERPOOL, YAIPIGA MAN CITY 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top