• HABARI MPYA

    Friday, October 14, 2022

    HALI HALISI AZAM FC KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA AKHDAR


    WACHEZAJI majeruhi Azam FC waliokosekana kwenye michezo iliyopita ukiwemo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Akhdar, wanaendelea vizuri.
    Ifuatavyo ni taarifa ya kitabibu kutoka kwa daktari wa timu.
    DANIEL AMOAH
    Aliumia msuli wa nyuma ya paja kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars.
    Kwa sasa anaendelea vizuri kwa 4/10 kutoka  9/10 alivyokuwa kabla. 
    Alianza mazoezi baada ya kurudi kutoka Libya akiwa na program ya peke yake. Huenda kesho Ijumaa akajiunga kwenye programu na wenzake.
    SOSPETER BAJANA
    Aliumia misuli ya sehemu ya ndani ya paja akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa nchini Libya.
    Alikosa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, akacheza mchezo dhidi ya Singida Big Stars na kujitoanesha.
    Anaendelea vizuri lakini hajaanza mazoezi.
    MALICKOU NDOYE
    Alichanika msuli wa nyuma wa paja kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
    Anaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi. Alianza peke yake kwa program maalumu na leo, Oktoba 13, amerejea kwenye mazoezi ya kawaida na wenzake.
    KENNETH MUGUNA
    Alichanika nyama ya paja kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya, El Gouna Misri.
    Akapona na kuanza kucheza lakini akajitonesha mazoezini.
    Kwa sasa anaendelea vizuri, alishaanza mazoezi ya peke yake na leo, Oktoba 13, amejiunga na wenzake mazoezini.
    AGREY MORIS
    Aliikosa safari ya Libya kutokana jeraha la goti.
    Lakini sasa amepona na anafanya mazoezi na wenzake.
    ABDALLAH KHERI
    Aliikosa safari ya Libya kwa sababu ya kuugua Malaria.
    Kwa sasa amepona na ameanza mazoezi na wenzake.
    IDD SELEMAN NADO
    Aliugua Malaria baada ya kurudi kutoka Libya. Amepumzishwa na anaendelea na matibabu.
    YAHYA ZAYD
    Baada ya kurejea safarini kutoka Libya, aliendelea na programu ya mazoezi kwa siku mbili, kabla ya leo Alhamisi kuugua malaria.
    Ameshindwa kufanya programu ya mazoezi leo, akiwa amepumzishwa huku akiendelea na matibabu.
    #weareazamfc #timuborabidhaabora
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HALI HALISI AZAM FC KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA AKHDAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top