• HABARI MPYA

  Monday, October 10, 2022

  SAKA APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA LIVERPOOL 3-2 EMIRATES


  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kimataifa wa England, Bukayo Saka amefunga mabao mawili kuiwezesha Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Saka alifunga dakika ya 45 na ushei akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza, Gabriel Martinelli dakika ya kwanza tu ya mchezo na la pili kwa penalti dakika ya 76.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Nunez dakika ya 34 na Roberto Firmino dakika ya 53.
  Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi moja zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi tisa, wakati Liverpool inabaki na pointi 10 za mechi nane nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKA APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA LIVERPOOL 3-2 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top