• HABARI MPYA

  Friday, October 07, 2022

  ARSENAL YAWAPAKIA WANORWAY MABAO 3-0 LONDON  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bodo/Glimt ya Norway katika mchezo wa Kundi A UEFA Europa League usiku huu Uwanja wa Emirates Jijini London. 
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah dakika ya 23, Rob Holding dakika ya 27 na Fabio Vieira dakika ya 84 na kwa ushindi huo katika mchezo wake wa pili, The Gunners inafikisha pointi sita na kupanda kileleni mwa Kundi, ikiizidi pointi mbili Bodø/Glimt iliyocheza mechi moja zaidi.
  Baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya wenyeji, FC Zurich sasa PSV nayo ina pointi nne katika nafasi ya tatu, ikizidiwa wastani wa mabao na Bodo/Glimt.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWAPAKIA WANORWAY MABAO 3-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top