• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2022

  YANGA YAWAFUATA AL HILAL SI KINYONGE

  KIKOSI cha Yanga kitaondoka Alfajiri ya kesho kwenda nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal Jumapili Jijini Khartoum. 

  Mechi yake kwanza Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na sasa inakabiliwa na mtihani wa kushinda ugenini.
  Haitakuwa mara ya kwanza Yanga kujikuta katika mtego wa kupigania ushindi ugenini – kwani mwaka 2001 katika michuano hii na hatua kama hii, Yanga ilitoa sare ya 2-2 na Highlanders FC ya Zimbabwe Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kushinda 2-1 Bulawayo katika mchezo wa marudiano mna kusonga mbele.
  Katika Hatua ya 16 Bora, Yanga ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 6-5, ikifungwa 3-2 Johannesburg na sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAWAFUATA AL HILAL SI KINYONGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top