• HABARI MPYA

  Sunday, October 30, 2022

  BRIGHTON YAIFUMUA CHELSEA 4-1 AMEX


  WENYEJI, Brighton & Hove Albion jana waliiadhibu Chelsea kwa kuitandika mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Amex,
  Mabao ya Brighton yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya tano, kabla ya wachezaji wawili wa Chelsea kujifunga Ruben Loftus-Cheek dakika ya 14 na Trevoh Chalobah dakika ya 42, huku bao la nne la wenyeji likifungwa Pascal Gross dakika ya 90 na ushei, wakati la kufutia machozi la The Blues lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 48.
  Kwa matokeo hayom, Brighton inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nane, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 21 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 12. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRIGHTON YAIFUMUA CHELSEA 4-1 AMEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top