• HABARI MPYA

  Tuesday, October 18, 2022

  KARIM BENZEMA ASHINDA BALLON D'OR 'UZEENI'


  MSHAMBULIAJI wa Real Madrid na Ufaransa, Karim Benzema amefanikiwa kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mwaka 2022, Ballon d'Or akiwa ana umri wa miaka 34.
  Katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Theatre Du Chatelet Jijini 
  Paris nchini Ufaransa usiku wa jana, Benzema alibeba tuzo hiyo akiwashinda Sadio Mane wa  Bayern Munich na Kevin De Bruyne wa  Manchester City.
  Mafanikio hayo yanafuatia Benzema kutoa mchango mkubwa kwa Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita huku pia akiendelea kufanya vizuri msimu huu.

  2022 BALLON D'OR AWARDS 

  Kopa Trophy: Gavi (Barcelona)

  Yashin Trophy: Thibaut Courtois (Real Madrid)

  Gerd Muller Award: Robert Lewandowski (Barcelona)

  Socrates Award: Sadio Mane (Bayern Munich)

  Ballon d'Or Feminin: Alexia Putellas (Barcelona)

  Club of the Year: Manchester City

  Ballon d'Or: Karim Benzema (Real Madrid) 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KARIM BENZEMA ASHINDA BALLON D'OR 'UZEENI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top