• HABARI MPYA

  Tuesday, October 18, 2022

  YANGA YAPEWA CLUB AFRICAIN ILIYOIPIGA KIPANGA 7-0

  KLABU ya Yanga itakutana na Club Africain ya Tunisia katika mechi ya mchujo wa kuwania kucheza Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Yanga itaanzia nyumbani Novemba 2, kabla ya kucheza mechi ya marudiano Tunisia Novemba 9. 
  Club Africain itakuwa inarejea Tanzania, kwani katia Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho iliitoa Kipanga ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 7-0, ikitoa suluhu Zanzibar kabla ya kwenda kutoa adhabu Tunis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPEWA CLUB AFRICAIN ILIYOIPIGA KIPANGA 7-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top