• HABARI MPYA

  Sunday, October 16, 2022

  SIMBA SC YATINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Simba SC leo limefungwa na mshambuliaji wake Mzambia, Mosea Phiri dakika ya 33 na sasa Wekundu wa Msimbazi wanakwenda Hatua ya Makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kuwafunga 3-1 Agosto kwao, Luanda wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top