TIMU ya Kipanga ya Zanzibar imetoa sare ya bila mabao na Club Africain ya Tunisia katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Amani, Zanzibar.
Timu hizo zitarudiana Oktoba 16, Jumapili ijayo Uwanja wa Olimpiki wa Radès mjini Radès, Tunisia na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na moja ya timu zilizotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
0 comments:
Post a Comment