• HABARI MPYA

  Tuesday, October 18, 2022

  SERENGETI GIRLS YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA


  TANZANIA imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia U17 licha ya sare ya 1-1 na Canada leo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Uwanja wa DY Patil Jijini Mumbai nchini India.
  Mechi nyingine ya kundi D leo, Japan iliichapa Ufaransa 2-0 hivyo kumaliza kileleni kwa ponti zake tisa, ikifuatiwa na Serengeti Girls pointi nne na Canada mbili. 
  Ufaransa, mabingwa wa zamani wa michuano hiyo ndio wameshika mkia kwa kuambulia pointi moja tu kwenye sare na Canada. 
  Katika Robo Fainali Jumamosi, Serengeti Girls watamenyana na Colombia na Japan watakipiga na Hispania, wakati Ijumaa Marekani itakutana na Nigeria na Ujerumani na Brazil.

  QUARTER-FINAL 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top