• HABARI MPYA

  Friday, October 07, 2022

  MSANII BEN POL AJA NA KAZI MPYA INAITWA ENJOYMENT


  MSANII  nguli wa muziki wa RnB, kinara wa Umoja wa Mataifa (UN), Balozi wa mazingira kitaifa kupitia ofisi ya Makamu wa Rais, Behnam “Ben Pol” Paul amekuja kivingine kupitia wimbo mpya uitwao Enjoyment aliyowashirikisha G Nako na Micky Singer ambao ameuachia Siku ya Ijumaa tarehe 7 Oktoba 2022.
  Wimbo umetayarishwa na studio za Fisher Records chini ya mtayarishaji Taz Goemi, na unapatikana kupitia redio na mitandao ya muziki nchini na duniani kote.
  Ben Pol amesema anafurahia kuweza kupata nafasi ya kufanya muziki pamoja na kuhudumia jamii kupitia mashirika kama UN, WildAid, WWF, Justdiggit, LEAD foundation ambayo amekuwa ni balozi wao. 
  “Ni jukumu langu kutumia ushawishi nilio nao kusaidia jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali ndio maana kuna kipindi nilikuwa Kimya kidogo, lakini sasa nawakaribisha kufurahia wimbo wangu mpya wa Enjoyment, Asante sana kwa support kwa wadau na mashabiki wangu wote” - Alisema Ben Pol.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSANII BEN POL AJA NA KAZI MPYA INAITWA ENJOYMENT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top