• HABARI MPYA

  Saturday, October 29, 2022

  TANZANIA PRISONS YAICHOMOLEA NAMUNGO DAKIKA YA MWISHO


  WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Namungo FC ilitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 21, kabla ya Frank John Magungi kujifunga akijaribu kuokoa shuti la Samson Mbangula na kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Tanzanian Prisons inafikisha pointi 13 nafasi ya saba na Namungo pointi 15 na kupanda nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHOMOLEA NAMUNGO DAKIKA YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top