• HABARI MPYA

    Sunday, May 08, 2022

    MAN CITY YAITANDIKA NEWCASTLE UNITED 5-0 ETIHAD



    WENYEJI, Manchester City wamepiga hatua moja mbele kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Newcastle United leo Uwanja wa Etihad, Manchester.
    Mabao ya Man City yamefungwa na Raheem Sterling mawili, dakika ya 19 na 90 na ushei, Aymeric Laporte dakika ya 38, Rodri dakika ya 61 na Philip Foden dakika ya 90 na kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 86 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 35.
    Newcastle United wao wanabaki na pointi zao 43 za mechi 36 sasa nafasi ya 13.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YAITANDIKA NEWCASTLE UNITED 5-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top