• HABARI MPYA

  Wednesday, May 11, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA ASTON VILLA 2-1


  TIMU ya Liverpool imeweka hai matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Aston Villa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Villa Park Birmingham.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Joel Matip dakika ya sita na Sadio Mane dakika ya 65 baada ya Aston Villa kutangulia kwa bao la  Douglas Luiz dakika ya tatu.
  Liverpool inafikisha pointi 86 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao na Manchester City ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Aston Villa yenyewe inabaki na pointi zake 43 za mechi 35 nafasi ya 11.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA ASTON VILLA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top