• HABARI MPYA

  Sunday, May 22, 2022

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SIMBA 1-1 KIRUMBA


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Dar es Salaam.
  Geita Gold walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake mahiri, George Enock Mpole dakika ya, kabla ya mshambuliaji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya 20 Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper kuisawazishia Simba dakika ya 28.
  Simba inafikisha pointi 51, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 12 na watani, Yanga, wakati Geita Gold inatimiza pointi 35, nayo inabaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SIMBA 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top