// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MECHI YA DODOMA JIJI NA YANGA SASA KUCHEZWA JIONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MECHI YA DODOMA JIJI NA YANGA SASA KUCHEZWA JIONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, May 14, 2022

  MECHI YA DODOMA JIJI NA YANGA SASA KUCHEZWA JIONI


  BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imerejesha nyuma muda wa kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Dodoma Jiji na Yanga Jumapili Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
  Taarifa kutoka idara ya habari na mawasiliano ya bodi ya ligi imesema mchezo huo uliokuwa uchezwe saa 1 kamili jioni Sasa utachezwa kuanzia saa 10 kamili za jioni.
  Taarifa hiyo imesema sababu za mchezo huo kurudishwa nyuma ni kupisha maandalizi ya shughuli nyingine itakayofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mei 16 ambapo maandalizi yake yanapaswa kukamilika usiku wa Mei 15.
  TPLB kupitia taarifa hiyo imesema vilabu vyote, maafisa na wadau wote wamejulishwa mabadiliko ya muda wa mchezo huo na tayari klabu ya Yanga imewasili jijini Dodoma tayari kwa mchezo huo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA DODOMA JIJI NA YANGA SASA KUCHEZWA JIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top