• HABARI MPYA

  Sunday, May 08, 2022

  KOLA APIGA ZOTE MBILI AZAM FC YAICHAPA KMC 2-1


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC leo yote yamefungwa na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola dakika ya pili na 36, wakati bao pekee la KMC limefungwa na Miraj Athumani dakika ya 48.
  Azam FC inafikisha pointi 32 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya tatu ikiiidi pointi moja Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 22, wakati KMC inabaki na pointi zake 24 za mechi 22 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOLA APIGA ZOTE MBILI AZAM FC YAICHAPA KMC 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top