• HABARI MPYA

  Thursday, May 12, 2022

  CHELSEA YAICHAPA LEEDS UNITED 3-0 ELLAND ROAD


  TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Elland Road, Leeds, West Yorkshire.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na  Mason Mount dakika ya nne, Christian Pulisic dakika ya 55 na Romelu Lukaku dakika ya 83 na sasa wanafikisha pointi 70 katika mchezo wa 36, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakiizidi pointi nne. Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Leeds United ambayo ilimpoteza mchezaji wake, Dan James aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 24 tu kwa kumchezea rafu Mateo Kovacic, inabaki na pointi zake 34 za mechi 36 nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA LEEDS UNITED 3-0 ELLAND ROAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top