• HABARI MPYA

  Friday, May 06, 2022

  NI RANGERS NA EINTRACHT FRANKFURT FAINALI EUROPA LEAGUE 2022


  TIMU ya Rangers ya Scotland imefanikiwa kwenda Fainali ya UEFA Europa Leagu baada ya ushindi wa 3-1 usiku wa Alhamisi Uwanja wa Ibrox Stadium Jijini Glasgow.
  Mabao ya Rangers yamefungwa na James Tavernier dakika ya 18, Glen Adjei Kamara dakika ya 24 na John Lundstram dakika ya 81, wakati bao pekee la RB Leipzig limefungwa na Christopher Nkunku dakika ya 70.
  Rangers wanakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mechi ya kwanza na sasa watamenyana na Eintracht Frankfurt  ya Ujerumani katika Fainali itakayopigwa Mei 18 Uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán Jijini Sevilla nchini Hispania.
  Eintracht Frankfurt iliichapa West Ham United 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Rafael Santos Borré Maury dakika ya 26 Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt am Main na kwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza London wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI RANGERS NA EINTRACHT FRANKFURT FAINALI EUROPA LEAGUE 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top