• HABARI MPYA

  Saturday, May 14, 2022

  LIVERPOOL YATWAA KOMBE LA FA BAADA YA MIAKA 16

   

  TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya miaka 16 kufuatia ushindi wa penalti 6-5 timu hizo zikitoka kumaliza dakika 120 bila kufungana Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Waliofunga penalti za Liverpool ni James Milner,  Thiago Alcântara, Roberto Firmino, Trent Alexander-Arnold, 
  Diogo Jota na  Konstantinos Tsimikas, huku Sadio Mane pekee akikosa mkwaju wake  ukiokolewa na kipa Msenegal mwenzake, Édouard Mendy.
  Upande wa Chelsea waliofunga ni Marcos Alonso, Reece James, Ross Barkley, Jorginho na Hakim Ziyech huku César Azpilicueta na Mason Mount wakikosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATWAA KOMBE LA FA BAADA YA MIAKA 16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top