• HABARI MPYA

  Thursday, May 12, 2022

  DE BRUYNE APIGA NNE MAN CITY YAICHAPA WOLVES 5-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameitandika Wolverhampton Wanderers mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Molineux, Wolverhampton, West Midlands.
  Nyota Mbelgiji, Kevin De Bruyne  peke yake amefunga mabao manne dakika za saba. 16, 24 na 60, kabla ya Raheem Sterling kufunga la tano dakika ya 84, wakati la Wolves limefungwa na Leander Dendoncker dakika ya 11.
  Man City imefikisha pointi 89, tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 36.
  Wolves wanabaki na pointi zao 50 za mechi 36 pia nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE APIGA NNE MAN CITY YAICHAPA WOLVES 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top