• HABARI MPYA

  Thursday, May 26, 2022

  TAIFA STARS KUANZA NA SOMALIA KUFUZU CHAN YA MWAKANI


  TANZANIA itaanzia ugenini kwa Somalia katika kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria.
  Mechi hiyo itachezwa kati ya Julai 22 na 24, kabla ya timu hizo kurudiana Tanzania kati ya Julai 29 na 31 katika mkoa utakaotajwa baadaye na mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba 2, mwaka huu.
  Fainali za CHAN ilikuwa zifanyike Julai 10 hadi Agosti 1, mwaka huu lakini Shirikisho la Soka (CAF) likasogeza hadi mwakani kutokana na kuahirishwa kwa fainali za zilizopita kusogezwa mbele sababu ya Janga la maambukizi ya virusi vya corona.


  Ikumbukwe mwezi ujao, Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
   
  Taifa Stars itakuwa mgeni wa Niger katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
  Baada ya Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUANZA NA SOMALIA KUFUZU CHAN YA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top