• HABARI MPYA

  Monday, May 23, 2022

  NAIBU WAZIRI AIPONGEZA SERENGETI GIRLS KWA USHINDI WA JANA


  NAIBU wa Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ameipongeza timu ya Taifa wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Cameroon jana katika mchezo wa kwanza Raundi ya mwisho kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17, baadaye mwaka huu nchini India.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana William dakika ya tatu na Clara Luvanga mengine yote matatu dakika za 29, 63 na 71 huku la wenyeji likifungwa na Mona Lamine dakika ya 26.
  Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Zanzibar, Serengeti Girls ikihitaji kuulinda ushindi wake ili kwenda India.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI AIPONGEZA SERENGETI GIRLS KWA USHINDI WA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top