• HABARI MPYA

  Friday, May 20, 2022

  NAMUNGO NA TANZANIA PRISONS SARE 3-3 LINDI


  WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Haruna Shamte dakika ya tano, Nurdine Chona aliyejifunga dakika ya 65 na Lucas Kikoti dakika ya 86, wakati ya Prisons yamefungwa na Ezekia Mwashilindi dakika ya nane, Jumanne Elfadhili kwa penalti dakika ya 56 na Moses Kitundu dakika ya 77.
  Kwa matokeo hayo, Namungo wanafikisha pointi 37 na kuendelea kushika nafasi ya tatu, wakati Tanzania Prisons wanafikisha pointi 24 na kusogea kwa nafasi moja juu hadi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO NA TANZANIA PRISONS SARE 3-3 LINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top