• HABARI MPYA

  Sunday, May 22, 2022

  MAN CITY BINGWA TENA ENGLAND, LIVERPOOL...


  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa mwisho leo Uwanja wa Emirates Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 76 na 81 na Rodri dakika ya 78 baada ya Villa kutangulia na mabao ya Matty Cash dakika ya 47 na Philippe Coutinho dakika ya 69.
  Manchester City inamaliza na pointi 93, ikiizidi pointi moja Liverpool baada ya mechi 38 za msimu.
  Liverpool imemaliza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Anfield katika nafasi ya pili.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 24, Mohamed Salah dakika ya 84 na Andrew Robertson dakika ya 89, baada ya baada ya Pedro Neto kuanza kuifungia Wolves dakika ya tatu.
  Chelsea imemaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na kufikisha pointi 74 mbele ya Tottenham Hotspur ya nne iliyomaliza na pointi 71 baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Norwich City.
  Arsenal imemaliza nafasi ya tano baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Emirates na kufikisha pointi 69.
  Manchester United imemaliza nafasi ya sita licha ya kuchapwa 1-0 na Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park Jijini London ikibaki na pointi zake 58.
  Burnley iliyomaliza na pointi 35, ikizidiwa tatu tu na Leeds United, imeungana na Watford na Norwich City kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu.
  Mohamed Salah wa Liverpool ndiye mfungaji Bora kwa mabao yake 22, mbele ya Son Heung-Min wa Tottenham aliyemaliza na mabao 21 na Cristiano Ronaldo wa Man Utd mabao 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY BINGWA TENA ENGLAND, LIVERPOOL... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top