• HABARI MPYA

  Monday, May 16, 2022

  FAINALI MICHUANO YA KLABU AFRIKA 2022 NI MOTO


  FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Afrika itazikutanisha Al Ahly ya Misri na Wydad Casablanca ya Morocco Mei 30 Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca.
  Aidha, Fainali ya Kombe la Shirikisho itazikutanisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini na RSB Berkane ya Morocco Mei 20 Uwanja wa Godswill Akpabio International mjini Uyo nchini Nigeria.
  Wydad Casablanca iliitoa Petro de Luanda kwa jumla 4-2 na Al Ahly imeitoa ES Sétif kwa jumla ya mabao 6-2.
  RSB Berkane ya kocha Mkongo, Flrent Ibenge imeitoa Mazembe ya DRC, kwa jumla ya mabao 4-2 na Orlando Pirates imeitoa Al Ahli Tripoli ya Libya kwa jumla ya mabao 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI MICHUANO YA KLABU AFRIKA 2022 NI MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top