• HABARI MPYA

  Monday, May 23, 2022

  BODI YAZIPONGEZA IHEFU NA DTB KUPANDA LIGI KUU


  BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imezipongeza KLABU za Ihefu SC ya Mbeya na DTB ya Dar es Salaam kwa kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
  Msimu wa Championship ulihitimishwa mwishoni mwa wiki, huku Mwadui FC na African Lyon zilizowahi kutamba katika Ligi Kuu zikiporomoka kwa ngazi nyingine kwenda chini, huku mabingwa Ihefu na washindi wa pili, DTB wakipanda moja kwa moja Ligi Kuu.  Kitayosce na JKT Tanzania zitakwenda kumenyana na timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 Ligi Kuu kuwania kupanda, huku Ken Gold, Mashujaa, Pamba FC, Fountain Gate, Green Warriors na Transit Camp zikijihakikishia kubaki Championship – na African Sports, Ndanda FC, Gwambina FC na Pan African zitamenyana na Daraja la Kwanza kuwania kubaki Championship.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BODI YAZIPONGEZA IHEFU NA DTB KUPANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top