• HABARI MPYA

  Sunday, May 08, 2022

  CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA WOLVES


  WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya 2-2 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumamosi Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na 
  Romelu Lukaku kwa penalti dakika ya 56 na 58 akimalizia pasi ya Christian Pulisic, wakati ya Wolves yamefungwa na Trincão dakika ya 79 na Conor Coady dakika ya 90 na ushei.
  Kwa sare hiyo, Chelsea inafikisha pointi 67 mechi ya 35, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Wolves imefikisha pointi 50 katika mechi ya 35 pia nafasi ya nane.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA WOLVES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top