• HABARI MPYA

  Wednesday, May 11, 2022

  MIKE TYSON ANUSURIKA MASHITAKA MAPYA MAREKANI

  BINGWA wa zamani wa ngumi za kulipwa uzito wa juu, Mike Tyson hatafunguliwa mashitaka baada ya kurekodiwa video inayoonyesha anampga ngumi abiria mwenzake wa first-class wakati ndege inaondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco mwezi uliopita.
  Ofisi ya Mwendesha Mashitaka District ya San Mateo County, amesema kesi imefutwa kutokana na utata mwingi kwenye tukio lenyewe – lakini baada ya maombi ya wahusika wenyewe. 
  Wawakilishi wa Tyson awali walisema bondia huyo wa zamani alikuwa kwenye ndege  na abiria mkorofi ambaye alianza kumsumbua akamtupia chupa ya maji akiwa ameketi kwenye siti yake.
  Aprili 20 video ilivuja ikimuonyesha Tyson akimpiga kichwani abiria mwenzake hadi akatokwa damu.


  Mike Tyson (kulia) akiwa na mkewe, Lakiha - maarufu kama  Kiki 

  Tyson anashikilia rekodi ya bingwa mdogo zaidi wa uzito wa juu duniani wa ngumi za kulipwa baada ya kutwaa taji hilo mwaka 1987 akiwa ana miaka 20 tu na kwa ujumla alishinda mapambano 50, kati ya hayo, 44 kwa Knockout.
  Miaka ya 1990, Tyson alitumikia kifongo cha miaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na tangu wakati huo amekuwa mtu muungwana katika Maisha yake.
  Tyson amewahi pia kufungiwa kwa muda kucheza ngumi mwaka 1997 baada ya kumng’ata sikio Evander Holyfield katika pambano baina yao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIKE TYSON ANUSURIKA MASHITAKA MAPYA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top