• HABARI MPYA

  Thursday, May 19, 2022

  TWIGA STARS KUANZA NA SUDAN KUSINI CECAFA CHALLENGE


  TANZANIA itafungua dimba na Sudan Kusini Juni 2 katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa FTC Njeru mjini Kampala, Uganda.
  Mechi ya pili ya Twiga Stars itafuatia Juni 4 dhidi ya Ethiopia, kabla ya kukamilisha mechi za Kundi hilo Juni 6 kwa kumenyana na ndugu zao, Zanzibar hapo hapo FTC Njeru.
  Nusu Fainali zitafuatia Juni 9 na Fainali pamoja na mechi ya kusaka mshindi wa tatu ni Juni 11 hapo hapo FTC Njeru.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS KUANZA NA SUDAN KUSINI CECAFA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top